ZIARA YA UTENDAJI KAZI YA KAMATI ZA MICHEZO MKOA WA LINDI
service image
29 Jan, 2024

Uongozi wa Mkoa wa Lindi umelipongeza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kazi nzuri inayoendelea kufanya ikiwemo kufuatilia utendaji kazi wa Kamati za Michezo Mkoa.

Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 29 Januari, 2024 na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Natalius Linuma mara baada ya kufanya kikao na maafisa michezo wa BMT, Mkoa na Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Kwa upande wake Afisa Michezo wa BMT Riziki Majala amesema lengo la ufuatiliaji wa Utendaji kazi wa Kamati za Michezo Mkoa ni kuhakikisha uratibu wa shughuli za kamati hizo zinafanya kazi kwa kufuata kanuni, taratibu na Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa sambamba na kukumbusha majukumu ya Kamati.