KIKAO CHA MAANDALIZI YA AWAMU YA PILI YA TUZO KWA WANAMICHEZO BORA
service image
28 Feb, 2024

Kamati ya usimamizi wa Tuzo za Michezo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT), leo tarehe 28.02.2024 imekaa kuweka mikakati kabambe kuelekea kwenye siku hiyo inayotarajiwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu.

Kamati hiyo inaundwa na Mwenyekiti ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa BMT Prof. Madundo Mtambo, Makamu mwenyekiti Leonard Thadeo Mkurugenzi wa michezo mstaafu, Katibu wa kamati Bi. Neema Msitha na Katibu Mtendaji wa Baraza, na wajumbe ni, Christinah Korosso Mkurugenzi Azam Media, Nassra J. Mohamed mwanamichezo mbobezi Juma Ikangaa mwanariadha mkongwe, Boniface Wambura kutoka TFF na Jonas Tiboroha Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam.