MAAGAZIZO YA RAIS KWA WIZARA

28 Jul, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha nchi inafanya maandalizi mazuri, ikiwemo kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu, viwanja viwili vipya vya kisasa vya michezo vitakavyojengwa mkoani Arusha na Dodoma.