WAZIRI MKUU ATOA RAI, 5% ITOKANAYO NA MICHEZO YA KUBASHIRI KUSAIDIA TIMU ZA TAIFA
service image
04 Oct, 2023

Nawaelekeza Wizara ya fedha asilimia 5 (%) inayotengwa kutokana na mchezo wa kubashiri kwa ajili ya Mfuko wa maendeleo ya michezo kusaidia timu za Taifa pamoja na fedha zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa ziwe zinafika kwa wakati ili ukarabati ukamilike kabla ya mashindano ya AFCON mwaka 2027 kwa kuwa nchi yetu ndio muandaji kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.

Rai hiyo ameitoa Oktoba 04, 2023 Jijini Dar es salaam katika tukio la kukabidhi Shilingi Milioni 500 kwa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars) ahadi ya Rais Dkt. Samia Suluhu kwa timu hiyo baada ya kufuzu mashindano ya AFCON 2027.