KUFUZU OLIMPIKI: CHANGALAWE KUPIMANA UWEZO NA MNORWAY.
service image
08 Mar, 2024

Bondia Yusuf Changalawe anatarajiwa kupanda ulingoni jioni ya leo Machi 08, 2024 dhidi ya Mindaugas Gedminas kutoka nchini Norway katika muendelezo wa mashindano ya kwanza ya Dunia ya kufuzu kushiriki michuano ya Olimpiki yanayotarajiwa kufanyika nchini Italia 2024.

Changalawe atapambana katika *Session 16B,* bout no. 393 ya uzani wa Light Heavyweight 80kg, hatua ya 32 bora ambapo mshindi wa pambalo hilo atafuzu katika hatua ya 16 bora na atapambana na mshindi wa bout no. 394 kati ya Pylyp Akilov (Hungary) au Lucky Aimufua (Austria)

Pambano *16*B linatarajiwa kuanza majira ya Tanzania saa 11.30 jioni na itaonyeshwa mubashara kupitia online streaming ya channel ya Olimpiki na Changalawe anatarajiwa kupanda ulingoni kuanzia majira ya saa 1.00 usiku.