SARS YAWEKEWA MIKAKATI MWANZA
service image
31 Jan, 2024

Maafisa Michezo na Utamaduni kutoka katika halmashauri nane (8) za Mkoa wa Mwanza tarehe 31 Januari, 2024 wamefanya kikao katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa huo kufanya tathmini ya matumizi ya mfumo mpya wa usajili kwa njia ya Kidigitali (SARS) pamoja na ushiriki wa wachezaji wa Mkoa huo katika michezo kwa mwaka 2023.

Aidha, sambamba na kufanya tathmini kikao hicho pia, kilitumika kuweka mikakati ya namna bora ya kushiriki kwa mafanikio katika mashindano mbalimbali yatakayofanyika katika mwaka 2024.

Mgeni rasmi katika kikao hicho, Afisa Elimu wa Mkoa wa Mwanza Mr. Martin Nkwabi aliwasisitiza Maafisa hao kujipanga vyema ili kuuwakilisha Mkoa huo kwa mafanikio makubwa katika mashindano watakayopeleka wachezaji yakiwemo ya UMITASHUMTA , UMISSETA na FEASSA.

"Ni imani yangu kuwa Halmashauri zote zina uwakilishi, Manispaa ya
Ilemela, Mwanza Jiji, Wilaya ya Misungwi,  Kwimba,  Magu, Sengerema, Ukerewe na
Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa,"aliwasisitiza

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Maafisa michezo Mkoa wa Mwanza Mr Kizito Bahati (Afisa michezo ilemela) alitumia fursa hiyo kuwakumbusha na kuwafundisha Maafisa michezo ambao hawakupata mafunzo ya namna ya kutumia mfumo wa usajili wa kidigitali (SARS) na kuwataka kuvisisitiza vyama kusajili kupitia mfumo huo kwani rahisi sana.

Naye Afisa Michezo Mkoa wa huo William James alisisitiza kuanzishwa kwa vitalu vya michezo (sports centre) katika kila kanda.