SERENGETI BOYS WAFUZU NUSU FAINALI YA AFCON U17
24 May, 2026
Timu ya Taifa ya Tanzania, Serengeti Boys, imeandika historia mpya kwenye soka la Afrika baada ya kufuzu hatua ya Nusu Fainali ya AFCON U17 ikiwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Hii ni hatua kubwa ambayo haijawahi kufikiwa na timu yoyote ya vijana wa chini ya miaka 17 nchini, na inaonesha maendeleo makubwa ya soka la vijana Tanzania.
Zaidi ya kufuzu Nusu Fainali, Serengeti Boys pia wameweka rekodi nyingine ya kihistoria kwa kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia la U17, linalotarajiwa kufanyika nchini Qatar mwezi Novemba 2026.

