SERIKALI NA HARAKATI ZA MAENDELEO YA MICHEZO
service image
26 May, 2022

Serikali kwa kushirikiana na Vyama vya michezo imeendelea kupambana kuhakikisha michezo ina litangaza vyema taifa kimataifa kupitia mashindano mbalimbali.
Hayo yamebainishwa leo Mei 26, 2022 na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Yusuph Singo wakati wa kikao na waandishi wa habari akieleza harakati hizo kupitia mashindano ya michezo tofauti yanayoendelea nchini.

Aliendelea kwa kusema tarehe 27 Mei, 2022 Serikali inatarajiwa kuzindua mashindano ya vijana ya mchezo wa Riadha wenye umri chini ya miaka 18 na chini ya miaka 20  ya Afrika Mashariki na Kati yatakayoshirikisha nchi saba, na yatahitishwa tarehe 28 Mei, 2022.
Alizitaja nchi hizo ambazo zimethibitisha kushiriki mashindano hayo ya vijana kuwa ni Sudan Kusini, Somalia, Kenya, Ethiopia, Eritrea, Zanzibar, pamoja na wenyeji Tanzania.

"Serikali imejipanga kuwekeza katika michezo hususani Kwa upande wa vijana ili kupata wanichezo mahiri, ndio lengo la kufanya haya mashindano hapa kwetu tunaomba watanzania waje kwa wingi kushuhudia vipaji vitakavyokuwa vinaonyeshwa na vijana wetu," alisema Singo.

Aliongeza kwa kusema kuwa tarehe hiyo hiyo 27 hadi 31 Mei, 2022 yatafanyika pia mashindano ya majaribio ngumi za riadhaa ya Afrika ambayo pia yatashirikisha nchi zaidi ya 6 kuwaandaa mabondia wa Tanzania kuelekea michezo ya Jumuiya ya Madola Julai - Agosti, 2022 nchini Uingerza.

Nchi zinazoshiriki katika mashindano hayo ni mwenyeji Tanzania, Uganda, Eswatini, Malawi, Burundi, Zambia, Msumbiji na Sudan Kusini.
Alisema kufuatia Serikali kujali michezo imeweza kuweka timu hiyo kambini kwa muda mrefu Ili kuhakikisha wanaridi na medali za ushindi.

Vile vile aliipongeza timu ya Taifa ya Base Ball 5 kufika hatua ya robo fainali katika michuano mikubwa ya mchezo wa Base Ball 5 Afrika ambayo yanafanyika kwenye uwanja wa ndani wa Taifa ikiwa mara ya kwanza kushiriki. Mashindano hayo yanayohitishwa leo Mei 26, 2022.
katika mashindano hayo ni Kenya, Uganda, Zambia, Tunisia, Afrika ya Kusini, Ghana, Burkina Faso, na mwenyeji Tanzania.