MASHABIKI SIMBA NA YANGA WATAKIWA KUHAMISHIA USHABIKI KWA TAIFA STARS
service image
29 Sep, 2023

SERIKALI imewataka mashabiki wa Yanga na Simba kuhamia kuziunga mkono timu za Taifa Ili kutoa hamasa ziweze kufanya vizuri .

Rai hiyo imetolewa leo Septemba, 2023 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa mkutano na waandishi baada ya kurejee kuisaka na kufuzu uwenyeji wa "Pamoja Afcon 2027" kati ya Kenya, Uganda na Tanzania.

Alisema kuwa wingi wa idadi kubwa ya mashabiki na hamasa ndio kigezo Cha Tanzania kupata fursa ya kupata nafasi ya ufunguzi au fainali ya Michuano Soka Barani Afrika (AFCON).

"Hamasa ya mpira wa Yanga na Simba imekuwa chachu kubwa na ndio maana CAF wameweka mechi ya ufunguzi wa 'Super League' dhidi ya Al Hilal itakaofanyika Oktoba 20 mwaka huu jijini Dar Es Salaam," alisema Dkt Ndumbaro.

Alisema Kuwa pamoja na hilo alizitaka Klabu hizo zisibweteke na waendeleaa kufanya mazoezi zaidi.

Aliongeza "wajibu wa Serikali na Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tayari tumeleta Afcon Sasa wajibu upo kwa watanzania;" alisema

Waziri huyo alisema kuwa wanaendelea kuweka nguvu ya maandalizi ikiwamo ya ujenzi wa viwanja kwa kuhakikisha vinakamilika mapema na kwa wakati.

Aliwapa wasaa sekta Binafsi kuhakikisha wanajipanga na kuchangamkia fursa hizo pindi timu zitakapowasili nchini zitahitaji huduma mbalimbali ikiwamo chakula, malazi na usafiri.

Wakati huo huo aliipongeza timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars Kwa kuidondosha Ivory Coast katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu WAFCON uliochezwa jumamosi iliyopita Dar Es Salaam.

"Safari bado haijaisha tuna mechi mbili za nyumbani na ugenini dhidi ya Togo na hii ni muhimu tufuzu WAFCON, tunataka baada ya kupata nafasi AFCON 2027 ",alibainisha Dkt Ndumbaro.

Naye Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia, alisema kuwa matayarisho yameanza na wana imani ya timu kufanya vizuri

Alisema Kuwa Tanzania itavaana dhidi ya Ivory Coast katika mchezo wa Afcon utakaofanyika Januari 2024 na kufuatiwa dhidi ya Morocco katika mchezo utakaochezwa Mwaka 2025 yatakuwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea Afcon 2027.