MAFUNZO YA MICHEZO KWA JAMII
service image
17 Jan, 2025

Nelson Kasiti (shati jeupe) mwakilishi wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Muheza Januari 17, 2025 alifunga mafunzo kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari wilayani Muheza Mkoani Tanga akiwataka wanufaika wa mafunzo hayo, yaende kuleta matokeo chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla, pamoja kuwashukuru Wakufunzi kutoka BMT kwa mafunzo yaliotukuka kwa walimu hao.

Mafunzo hayo yanawezeshwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania.