TANZANIA NA IRELAND KUSHIRIKIANA KATIKA UTAMADUNI NA MICHEZO

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na Balozi wa Ireland hapa nchini Mhe. Mary O' Neill na kukukubaliana kushirikiana katika Sekta ya michezo hususan soka la Wanawake pamoja na Sekta ya Sanaa katika eneo la uchoraji.
Katika Mazungumzo yao yaliyofanyika leo Septemba 22, 2023 ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam, Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro aliwasilisha ombi kwa nchi hiyo kusaidia kutoa mafunzo kwa watalaamu wa michezo hapa nchini katika eneo la usimamizi wa miundombinu ya michezo pamoja na wataalamu wakufundisha michezo.
"Nawakaribisha pia katika nchi yetu muweze kufanya maandalizi ya misimu ya ligi zenu kwakuwa nchi yetu ina maeneo mazuri katika maeneo ya Dar es Salaam Kigamboni, Tanga, Arusha na Zanzibar naamini mtafurahia sana. Na kwasasa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya Miaka 17 ya nchini Morocco ipo hapa nchini ikiwa inacheza mechi za kirafiki na timu yetu ya umri huo"amesema Mhe. Ndumbaro.
Awali Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Saidi Yakubu ameikaribisha nchi hiyo kupitia Ubalozi huo kushirikiana na Chuo cha Michezo Malya katika kutoa mafunzo kwenye fani zinazotolewa chuoni hapo