TANZANIA YATOKA SARE NA NIGERIA KRIKETI
service image
08 Mar, 2024

Mashindano ya Afrika ( All African Games 2023) yameanza kutimua vumbi jijini Accra, Ghana ambapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa mapema Machi 7, 2024 Timu ya Taifa ya Tanzania ya Kriketi iligawana alama moja na Nigeria baada ya mchezo huo kutochezwa kutokana na mvua kubwa kunyesha iliyopelekea mchezo huo kuahirishwa.

Mchezo wa pili dhidi ya Afrika Kusini umechezwa leo machi 8, 2024 ambapo Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ameongoza Watanzania walio nchini Ghana kushuhudia mchezo huo, ambapo Tanzania imepoteza na kuifanya iendelee kuwa na alama moja hadi sasa.

Michezo mingine itaanza kutimua vumbi mara baada ya ufunguzi rasmi wa mashindano hayo leo.