TANZANIA YATOA SARE NA UGANDA
service image
10 Mar, 2024


Mchezo wa Mpira wa Miguu kwa Wanawake chini ya miaka 20 uliochezwa machi 9, 2024 ikiwa ni mchezo wa kwanza wa wawakilishi hao wa Tanzania upande wa mchezo wa mpira wa miguu kwenye mashindano ya All African Games yanayoendelea nchini Ghana, ambapo Tanzania imetoka sare ya goli moja dhidi ya Uganda.

Mechi hiyo imechezwa Uwanja wa Cap Coast Machi 11, 2024 ambapo mechi nyingine inatarajiwa kuchezwa machi 10, 2024 dhidi Ghana.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 54 za Afrika ambazo zinashiriki mashindano hayo yenye jumla ya michezo 29.