TANZANIA YAWEKA HISTORIA, YAFUZU HATUA YA 16 BORA AFCON KWA MARA YA KWANZA
30 Dec, 2025
Tanzania imeandika historia mpya katika soka la Afrika baada ya Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) kufuzu hatua ya 16 bora ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Historia hiyo imepatikana baada ya Taifa Stars kutoka sare ya bao 1–1 dhidi ya Tunisia katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi uliopigwa nchini Morocco. Bao la Tanzania limefungwa na Feisal Salum.
Kufuzu hatua ya 16 bora ni hatua kubwa kwa maendeleo ya soka la Tanzania, na kunatoa ujumbe wazi kuwa Taifa Stars sasa ni timu ya ushindani barani Afrika. Mafanikio haya yanatarajiwa kuongeza hamasa, imani na uwekezaji katika mchezo wa mpira wa miguu nchini

