WATANZANIA FANYENI MAZOEZI KUIMARISHA AFYA YA MWILI
service image
30 Dec, 2023

Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Balozi Dokta Pindi Chana amewataka watanzania kufanya mazoezi ili kuimarisha afya ya mwili na kuepuka magonjwa yasiyoambukiza.

Mhe. Chana ameyasema hayo leo tarehe 30 Disemba, 2023 katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es Salaam, alipokuwa anazindua mbio za Ushirikiano baina ya Tanzania na India, zilizoandaliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania kwa kushirikiana na wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) pamoja na Shirikisho la Riadha Tanzania.

"watanzania safi, mheshimiwa Rais Samia Suluhu safi, kwanza kabisa niwapongeze sana waandaaji wa mbio hizi Ubalozi wa India nchini Tanzania, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na RT kwa kufanikisha jambo hili, mazoezi ni afya hivyo niwaombe watanzania wenzangu tuwe na mazoea ya kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zetu na kuepukana na magonjwa mbalimbali," amesema Balozi Pindi Chana.

Mbio hizo zinafanyika kwa kilomita 5, 10 na 60 kuanzia Dar es Salaam mpaka Bagamoyo mkoani Pwani.