WATANZANIA UNGENI MKONO JUHUDI ZA SERIKALI SEKTA YA MICHEZO
service image
10 Jan, 2024

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro, amewataka watanzania kuendelea kuunga mkono maendeleo ya sekta ya michezo katika harambee ya kuchangia timu za Taifa itakayofanyika tarehe 10 Januari, 2024 Jijini Dar es salaam.

Hafla hiyo ya awamu ya kwanza itafanyika katika hoteli ya Johari Rotana Dar Es Salaam na kushuhudia kwa njia ya mtandao na Rais wa Samia Hassan Suluhu ambaye atakuwa mgeni rasmi na atawakilishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa .

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Januari 09, 2024, Waziri Ndumbaro, alisema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia timu za taifa ambazo zinatarajia kushiriki michuano ya Kimataifa ikiwemo 'All African Games' Afcon kwa wanawake Olimpiki ambapo hadi sasa timu tatu zilizofuzu ikiwemo Riadha, Ngumi na soka la wanawake zenye uhakika.

Alisema kuwa harambee hiyo itafanyika katika robo nne za mwaka huku awamu nyingine zitafanyika nje ya Dar es Salaam na kuwataka Wakuu wa mikoa kuandika maombi kupitia Tamisemi wapate nafasi ya kufanya harambee hiyo katika Mikoa yao.

" Kamati ya hamasa imechaguliwa ambayo itafanya kazi hiyo Kwa mwaka mzima , kwani mwaka huu yapo matukio matano ya kuanzia mwezi huu, kwahiyo harambee hii itafanyika kwa awamu nne," alisema Waziri Ndumbaro.