TBC, TSN NA BMT ZAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE
23 Jan, 2026
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Husna Sekiboko imekamilisha kazi yake kwa mepokea na kujadili taarifa za Taasisi tatu za wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Taaarifa hizo ambazo ziliwasilishwa leo Januari 22, 2026 Bungeni jijiji Dodoma na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma ni ya Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC), Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

