TENGA: PAMOJA NA NIA NJEMA YA SERIKALI LAZIMA TUSHIRIKISHE SEKTA BINAFSI.
service image
20 Jul, 2023

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Leodiegar Tenga amewataka viongozi wa vyama vya michezo kuwahamasisha wawekezaji kuwekeza katika michezo ili kuisaidia Serikali pamoja na uwekezaji iliyofanya katika sekta hiyo.

Haya ameyasema Julai 20, 2023 katika tukio la Mafunzo kwa viongozi wa vyama vya michezo na uzinduzi wa mfumo wa usajili kidigitali yaliyoratibiwa na BMT Dar es salaam.

*Michezo inahitaji nyenzo, inahitaji rasilimali kubwa sana, na rasilimali hizi haziwezi kutoka serikalini peke yake, na nchi nyingi zilizofanikiwa katika michezo zimeshirikisha sekta binafsi,"alisema.

"Hatuwezi kurudi nyuma lazima tuwashawishi wadhamini kuwekeza katika michezo yetu, michezo ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya nchi," alisisitiza Tenga.