TENGA : NGUVU YENU IPO KWENYE USHIRIKIANO
service image
29 Apr, 2025

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mhandisi Leodigar Chilla Tenga ameitaka sekretarieti ya Baraza kuendelea kushirikiana ili kuendelea kuiimarisha taasisi hiyo ya michezo nchini.

Hayo ameyasema April 29, 2025 wakati wakijadiliana mambo kadhaa na Wajumbe wenzake pamoja na Menejimenti ya wakiwa katika kikao chao cha mwisho Baraza hilo.

"Nguvu yenu ipo kwenye ushirikiano, naomba mlipe kipaumbele,"amesisitiza.

Baraza hilo limefikia tamati kwa mujibu wa miongozo ya serikali ila kikao rasmi cha kuwaaga kitafanyika baadaye kutambua mchango wao katika Baraza hilo.