SERIKALI YAPONGEZA TIMU ZILIZOSHIRIKI MASHINDANO YA AFRIKA
service image
25 Mar, 2024

Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT), limezipongeza timu zote za Taifa zilizoshiriki katika mashindano ya Afrika (All African Games) kuanzia tarehe 8 hadi 23 Machi, 2024 jijini Accra nchini Ghana na kufanikiwa kupata medali tatu (3) za Shaba kutoka katika mchezo wa ngumi.

Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Michezo wa BMT Nicholaus Mihayo, baada ya kuupokea msafara wa Timu uliowasili tarehe 25 Machi, 2024 saa 9:30 alfariji katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere III, ambapo amesema kuwa timu ya Taifa ya ngumi imeonyesha mfano wa kuigwa katika mashindano hayo baada ya miaka mingi kupita.

Aidha Mihayo amezitaka timu nyingine ambazo hazikufanya vizuri,kuendelea kufanya mazoezi kwa bidii, ili kuweza kufanya vizuri katika mashindano yajayo ya kimataifa.