AHADI YA MHE. RAIS KWA TAIFA STARS YAWASILISHWA RASMI
service image
04 Oct, 2023

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akabidhi hundi ya Shilingi Milioni 500 ya Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) Ndg. Wallace Karia (kulia) ikiwa ni ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa kwa Timu hiyo, baada ya kufuzu kucheza Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2023 yatakayofanyika nchini Ivory Coast mapema mwaka 2024. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo Oktoba 04, 2023 alikuwa shuhuda wakati Waziri Mkuu akikabidhi hundi hiyo kwa Rais Karia katika Uwanja wa Benjamin Jijini Dar es salaam.