TAMASHA LA MICHEZO LA WANAWAKE 2023
08 Sep, 2023
Awamu ya tatu ya Tamasha la michezo la Wanawake kufanyika Oktoba 2023
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la michezo kwa wanawake (Tanzanite) leo Septemba 08, 2023 ameongoza kikao cha kwanza cha Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kwa awamu ya tatu (3) mwezi 0ktoba, 2023 Jijini Dar es salaam.
Tamasha la mwaka huu linalotarajiwa kufanyika kwa siku mbili (2) ambalo litahusisha mechi kali ya mpira wa miguu ya wanawake kwa siku ya kwanza ikifuatiwa na Kongamano kabambe litakalokuwa na mada mahususi kwa mustakabali wa kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo sambamba na tuzo kwa wanawake waliofanya vizuri katika sekta ya michezo.