TPSA YAPATA VIONGOZI WAPYA.

Chama cha mchezo wa Kuogelea kwa watu wenye Ulemavu Tanzania (TPSA) umepata Viongozi wapya katika uchaguzi Mkuu uliofanyika April 6, 2025 Kwenye ukumbi wa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao watadumu kwa kukiongoza Chama hicho kwa miaka minne kuanzia Sasa.
Nafasi ya Mwenyekiti ni Thauria Diria,huku Clara Kizigha akiwapata nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Nafasi nyingine Katibu Mkuu ni Ramadhan Namkoveka ,huku Edgar Makwani Mlenge akichukua nafasi ya Mweka hazina.
Mkurugenzi wa Ufundi ni Julius Felix Maganga,wakati nafasi ya Mkurugenzi Mafunzo imechukuliwa na Innocent Jonas na Mjumbe ni Bijal Dipak Lal.
Akizungumza Mara baada ya kutangaza washindi hao Mwenyekiti wa Uchaguzi Apansia Lema amewataka kuhakikisha wanasajili na kuunda klabu sanjari na na vilivyopo ambavyo havijasajiliwa visajiliwe.
Amesema kuwa kuhakikisha wanajaza nafasi mbili za wajumbe ambazo bado zipo wazi
"Viongozi wote kila mmoja asimame katika nafasi yake kwa kuangalia na kutekekeza majukumu yake Kwa mujibu wa katiba," amesema