TWENDE OLIMPIKI 2024
service image
20 Apr, 2024

Baadhi wa watumishi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo tarehe 20 Aprili,2024 wameshiriki katika mbio ya Twende Olimpiki 2024 (5Km FunRun) zilizoandaliwa na ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).

Mbio hiyo ilianzia katika Shule ya Ufaransa (Arthur Rimbaud) Masaki na kuishia katika kituo cha Utamaduni wa Ufaransa (Alliance France) Upanga zikiwa zimebaki takribani siku 100 kufanyika kwa michezo ya Olimpiki jijini Paris nchini Ufaransa.