U17 YAFUZU FAINALI
service image
29 Apr, 2023

Timu ya Wasichana chini ya miaka 17 ya Mpira wa Mikono ya Tanzania imefanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya Mashindano ya kanda ya Tano Afrika yanayoendelea kwenye Uwanja wa Ndani wa Mkapa Jijini Dar es salaam.

Tanzania imefanikiwa kufuzu hatua hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 30-18 dhidi ya Kenya katika mchezo uliochezwa jana kwenye Uwanja huo.

Mashindano hayo yanashirikisha Timu za Wasichana U17 na U19 kutoka Mataifa wanachama kanda ya Tano.

Bingwa wa mashindano hayo katika Umri huo ataiwakilisha kanda hiyo kwa kwenda kupambana na kanda zingine kumpata bingwa wa Afrika.