UKARABATI WA UWANJA WA MKAPA UNAENDELEA KWA KASI.
service image
15 Apr, 2024

Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Milinde Mahona amesema ukarabati unaoendelea hivi sasa ni kukarabati eneo la kukimbilia mchezo wa riadha kwa kubadilisha kapeti la zamani.

"Ukiangalia kwa makini utaona kapeti la zamani lilipoteza ubora hivyo sasa ni wakati wa kufanya marekebisho kwa kuweka kitu kipya ili kuweka mazingira bora.

"Ukarabati ulianza mwezi Agosti mwaka jana kwa kurekebisha miundombinu mbalimbali ikiwamo eneo la kuchezea mpira wa miguu, kubadilisha spika pamoja na mfumo wa maji taka kwa maeneo ambayo yalikuwa na changamoto.



"Lakini pia hata kwenye chumba cha mikutano ya waandishi wa habari pia inafanyiwa ukarabati kwa kutoa mifumo ya zamani ya kupambana na moto pamoja miundombinu mingine ambayo iliacha kufanya kazi.

Alisema kuwa maboresho haya hayawezi kuzuia mchezo ujao wa watani wa jadi Simba na Yanga utakaopigwa Aprili 20 kwani sehemu muhimu zinazohusika na mchezo huo ziko vizuri