UONGOZI MPYA WA JUDO TANZANIA WAKABIDHIWA OFISI RASMI
Uongozi mpya wa Chama cha Mchezo wa Judo Tanzania umekabidhiwa rasmi ofisi, makabidhiano yalifanyika chini ya Rais mpya aliyechaguliwa, Bw. Richard Marton Ndayirukiye, pamoja na Katibu wa Chama aliyemaliza muda wake wa uongozi, Bw. Innocent Marya.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT), yakishuhudiwa na Afisa Michezo Mwandamizi, Bw. Charles Maguzu. Tukio hilo limeelezwa kuwa ni hatua muhimu katika kuanza rasmi kwa utekelezaji wa majukumu ya uongozi mpya wa chama hicho.
Katika makabidhiano hayo, viongozi wapya wametakiwa kuendeleza juhudi za kuuboresha na kuukuza mchezo wa Judo nchini Tanzania, sambamba na kuimarisha ushirikiano na viongozi waliopita, ili kuhakikisha maendeleo endelevu ya mchezo huo kuanzia ngazi za msingi hadi kitaifa.

