USAILI WA KUWAPATA VIONGOZI WA KAMATI YA PARALIMPIKI TANZANIA (TPC)
service image
24 Jan, 2026

Usaili wa kuwapata viongozi wa Kamati ya Paralimpiki Tanzania (TPC) umefanyika leo, Januari 24, 2026, katika ukumbi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Aidha uchaguzi wa kuwapata viongozi wa Kamati ya Paralimpiki Tanzania utafanyika tarehe 25 Januari, 2026, katika ukumbi huo huo wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Mchakato huu unalenga kuhakikisha TPC inapata uongozi madhubuti, wenye uwezo na dira ya kuendeleza michezo ya Paralimpiki, kulinda maslahi ya wanamichezo wenye ulemavu na kuinua heshima ya Tanzania katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.