VIPAJI KUENDELEZWA

21 Sep, 2022
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetakiwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Michezo kuandaa mfumo wa kutafuta vipaji vya wanamichezo wa michezo tofauti pamoja na kuviendeleza.
Rai hiyo imetolewa na Waziri mwenye dhamana ya michezo Mohamed Septemba 21, 2022 wakati wa tukio la kuiaga na kuikabidhi bendera timu ya wanawake mpira wa miguu chini ya umri wa miaka 17 'Serenget Girls' (U 17) ambayo inatarajia kusafiri tarehe 25 kuelekea nchini Uingereza katika kambi yao ya mwisho kabla ya kuelekea nchini India Oktoba katika michuano ya kombe la dunia.