VIPAJI VYA RIADHA VYAENDELEA KUIBULIWA UMITASHUMTA
service image
08 Jun, 2023

Siku ya pili ya kuibua vipaji vya riadha katika mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) imeendelea kupamba moto huku wanafunzi wa shule za msingi kutoka katika Mikoa tofauti nchini wakionesha vipaji vyao katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya wanaume ya Tabora (Tabora Boys).

Mchezo wa riadha ni moja katika michezo inayoendelea kuing'arisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya kimataifa lakini pia ni mchezo ambao umeiletea medali ya kwanza kupitia kwa mwanamama Theresia Dismas katika kurusha kisahani katika mashindano ya All African Game mwaka 1965.

Mashindano ya umitashumta yameanza Juni 03 na kufunguliwa rasmi na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango Juni 06, 2023 katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Mkoani Tabora.