WAAMUZI WA MPIRA WA WAVU ZINGATIENI KANUNI NA SHERIA ZA MASHINDANO.
service image
05 Aug, 2022

Kaimu Mkurugenzi wa Miundo mbinu kutoka wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Makoye Alex Nkenyenge, amewataka waamuzi, wachezaji na makocha kuzingatia kanuni na Sheria za mashindano ya mpira wa Wavu ngazi ya Taifa, ili kupata timu bora ya Taifa itakayoleta ushindani na kufanya vizuri katika michezo ya kimataifa.

Nkenyenge ametoa rai hiyo tarehe 04 Agosti, 2022 alipokuwa anafungua mashindano ya mpira wa Wavu Ligi ya Taifa.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) Mhandisi Magoti Mtani,amesema kuwa ligi hiyo itafanyika kwa mizunguko mitatu, ambapo wa kwanza umeanza Agosti,Septemba na kumalizika Oktoba mwaka huu.

" Katika hili TAVA kwa kushirikiana na BMT pamoja Azam tumedhamiria kurudisha mchezo kwa mashabiki,tupo tayari na milango ipo wazi kwa wadau waje kutuunga mkono kuinua mchezo huu," alisema Mhandisi Mtani.