WACHEZAJI WA TANZANIA WAENDELEA KUNG’ARA MASHINDANO YA WAZI YA GOFU WANAWAKE 2023.
service image
16 Sep, 2023

Wachezaji wa Tanzania wakiongozwa na mchezaji mwenye kiwango bora barani Afrika katika mchezo wa Gofu wanawake Madina Iddi, Vicky Elias, Hawa Wanyeche na Neema Olomi, wameendelea kuiperurusha vyema Bendera ya Taifa dhidi ya wachezaji kutoka nchini Kenya na Uganda katika mashindano ya wazi ya Gofu wanawake yanayoendelea katika viwanja vya Kiligolf Estate mkoani Arusha.

Mashindano hayo yaliyoanza tarehe 15 Septemba, yatafikia tamati tarehe 17 Septemba, 2023.