Dkt. Abbas: Ameupiga mwingi
service image
05 Apr, 2022

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. hassan Abbasi akiwasilisha mada ya namna gani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alivyoupiga mwingi na kuondoka nao ndani ya mwaka mmoja wa utawala wake katika sekta ya Utamduni na Michezo.

Mada aliyoiwasalisha leo Aprili 05, 2022 katika kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo kinachofanyika kwa siku tatu (3) kuanzia tarehe 04 hadi 06, Aprili, 2022 Jijini Dodoma.

Aidha, Dkt. Abbasi katika mada yake hiyo amewaeleza maafisa hao namna Mhe. Rais alivyowezesha maendeleo ya sekta hizo katika masuala mbalimbali ikiwemo kuwezesha kufanyika kwa Mashindano.ya kimataifa, wachezaji na timu kushiriki katika mashindano ya kimataifa na kurudi na ushindi, kuwezesha maandalizi ya timu, pamoja na maboresho na ujenzi miundombinu ya michezo.