KATOTO KAMA KAWAIDA KAMCHAKAZA MMISRI KWA POINTS 5-0
service image
11 Sep, 2023

Bondia machachari Abdallah Abdallah *"KATOTO"* amefanikiwa kushinda kwa kishindo dhidi ya mpinzani wake Abdallah Saied Nasser EMAM kutoka Misri kwa points za majaji wote watano (5-0) katika uzani wa 51kg ya bout no. 114.

Sasa jumla ya Watanzania 3 wametinga hatua za robo fainali akiwepo Yusuf Changalawe, Grace Mwakamele na Katoto.

Bondia mwingine wa Tanzania aliyecheza leo awali Musa Maregesi alipoteza kwa points dhidi ya mwenyeji kutoka Senegal Kebe Karamba katika uzani wa 92kg ya bout.l no 99.

Kesho ni siku ya mapumziko katika michezo hii ya kuwania nafasi za kufuzu kushiriki Olimpiki ya Paris 2024 inayoendelea Dakar, Senegal.