MAANDALIZI YA TANZANITE YAPAMBA MOTO

Maandalizi kuelekea kwenye tamasha la pili la michezo kwa wanawake lijulikanalo kwa jina la madini yenye dhamani ya Tanzanite limepamba moto, ambalo linatarajiwa kufanyika mwisho mwa mwezi huu Septemba kuanzia tarehe 28 hadi tarehe 30 Jijini Dar es salaam.
Akizungumza leo Septemba 13, 2022 katika kikao na kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha ameeleza kuwa tamasha la mwaka huu litafana kuliko la mwaka jana kwakuwa litahusisha baadhi ya michezo kimataifa ikiwemo Netiboli na Mpira wa miguu.
Michezo mingine itakayochezwa katika tamasha hilo ni pamoja riadha, mpira wa wavu, mpira wa kikapu, karate, kabaddi, mchezo wa kunyanyua vitu vizito, ngumi za kulipwa na ridhaa.
Tamasha litahusisha pia, wanamuziki mbalimbali kuvutia watu watazamaji lakini pia kuleta hamasha kwa wachezaji.