MASHINDANO YA RIADHA KWA WANAWAKE YAREJEE TENA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha mpambanaji katika kuhakikisha michezo nchini inakua pamoja na kuona wanawake wanashiriki kikamilifu, leo tarehe 13 Septemba, 2022 katika vikao vyake amekaa na wawakilishi wa shirika la ushirikiano wa kimataifa la Japan (JICA) kupanga mikakati ya kurejee kwa mashindano ya riadha kwa wanawake 'Ladies First' yaliyositishwa kufanyika kipindi cha Corona.
Mashindano ya Wanawake ya Riadha (LadyFirst) yamepangwa kufanyika Januari 28 na 29, 2023 kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yanaandaliwa kwa ushirikiano wa JICA kwa kushirikiana Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Akizungumza katika kikao cha Kamatihichi cha maandalizi ya mashindano hayo Mwakilishi JICA Naofumi Yamamura, alisema wanategemea kushirikisha washiriki 189 kutoka mikoa 31 ya Tanzania.
Ametaja mbio zitakazohisika katika mashindano hayo kuwa ni, mita 100, 200, 400, 800, 1500, 5000, 10,000 na mita 100 × 4 relay.
"lengo ni kutoa fursa kwa Wanawake kushiriki katika ridhaa na kuwepo na usawa katika ushiriki wa Tanzania kushawishi kutangaza michezo kwa maendeleo nchini,
"amesema Yamamura.