MHE.MCHENGERWA: SEKTA YA MICHEZO NCHINI INAENDELEA KUIMARIKA
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Omari Mchengerwa ameeleza kuwa, Sekta ya michezo nchini imeendelea kuimarika na imechangia zaidi ya shilingi Bilioni 1.7 katika pato la Taifa na Wizara imeendelea kujipanga ili kuhakikisha mchango wa Sekta hiyo unafikisha shilingi Bilioni 3 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Hayo ameyabainisha tarehe 05 Aprili, 2022 wakati wa hotuba yake kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kufungua kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo kinachofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 04 - 06 mwezi huu Jijini Dodoma.
“Wizara imeendelea na mikakati ya kufanya maboresho ya miundombinu ya michezo, na hapa ni pamoja na maboresho ya ujenzi wa viwanja vya michezo katika shule 56 ambapo kila Mkoa utakuwa an Shule mbili za michezo, ikienda sambamba na uanzishwaji wa mkakati wa kuibua vipaji wa mtaa kwa mtaa.”