TANZANIA YAPOTEZA KWA MAGOLI 40-31 DHIDI YA POLISI MALAWI.
service image
08 Sep, 2022

        Timu ya mchezo wa Netiboli ya Polisi Tanzania leo tarehe 08 Septemba, 2022 imeshuka dimbani kucheza na Timu ya Polisi Malawi na kukubali kufungwa magoli 40-31, mchezo uliochezwa uwanja wa Netiboli wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, katika mashindano ya Majeshi ya Polisi ukanda wa Kusini mwa Aftika yanayoendelea kutimua vumbi hapa nchini.

Kwa upande wa matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa, Timu ya Polisi ya Eswatin nayo imekubali kufungwa na timu ya Polisi ya Zimbabwe kwa magoli 43-33 huku Polisi Zambia ikiichapa Polisi Namibia kwa magoli 62-30.