TPBRC WATAKIWA KUWASILISHA TAARIFA YA SAFARI YA MWAKINYO MWISHO SEPTEMBA 13.
service image
09 Aug, 2022

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha ameuagiza uongozi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) kuwasilisha taarifa ya safari ya bondia Hassan Mwakinyo nchini Uingereza mwisho siku ya Jumanne Septemba 13, 2022.

Agizo hilo amelitoa leo Septemba 09, 2022 alipowaita viongozi wa Kamisheni hiyo inayosimamia ngumi za kulipwa nchini na kufanya nao mazungumzo juu ya safari ya bondia huyo, kikao kilichofanyika Ofisi kwake Jijini Dar es salaam.

Kikao hicho ni kufuatia maelekezo ya Mhe. Waziri mwenye dhamana ya michezo Mohamed Mchengerwa aliyotoa Septemba 06 na kuwaagiza BMT kukutana na baadhi ya vyama na kumpa taarifa ya sintofahamu kwa wanamichezo wanaposhiriki mashindano ya kimataifa.

Aidha, Msitha katika kikao hicho amewataka viongozi hao wa TPBRC na wa vyama vingine kuhakikisha wanasimamia ipasavyo taratibu zilizowekwa kuendesha michezo nchini bila kumwonea mchezaji au wachezaji.

"Hakikisheni mnasimamia taratibu zilizowekwa na nchi bila kumwonea mchezaji au wachezaji,"alisisitiza.

Nao viongozi wa TPBRC akiwemo Rais Chaurembo Palasa, Makamu wake Agapito Basil na Katibu Mkuu Yahya Poli wamemhakikishia Mtendaji Mkuu BMT kuwa taarifa hiyo