VIONGOZI WASILISHENI MAJINA YA WACHEZAJI MAPEMA

Viongozi wa vyama vya michezo itakayoshiriki mashindano ya wanawake (Tanzanite) yanayoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), wametakiwa kuwasilisha majina ya wachezaji wao watakaoshiriki katika mashindano hayo ifikapo tarehe 19 Septemba, 2022 ili kuendana na kasi ya maandalizi ya mashindano.
Wito huo umetolewa leo tarehe 15 Septemba, 2022 na kamati ya kuratibu mashindano ya Tanzanite,inayoongozwa na mwenyekiti Dokta Christine Luambano, baada ya kukaa kikao na viongozi hao kujadili namna bora ya kufanikisha mashindano pamoja na kujua idadi kamili ya wachezaji na viongozi watakaoshiriki.
“wasilisheni mapema majina ya wachezaji wenu watakaoshiriki Tanzanite, ifikapo tarehe 19 Septemba, majina yote yawe yametufikia kamati,hii itatusaidia tuendane na kasi ya maadnalizi ya mashindano yetu,”alisema Dkt. Luambano.
Kwa upande wa michezo ambayo itachezwa katika mashindano ya Tanzanite ni pamoja na mchezo wa Riadha, Karate, Netiboli, Ngumi za wazi, Ngumi za kulipwa, Kabaddi,Michezo ya Jadi, Mpira wa kikapu kwa walemavu pamoja na Mpira wa mikono.